Waziri
wa habari,Vijana,utamaduni na michezo Dr Fenella Mukangara akitangaza
majina ya wanakamati aliowateuwa kuratibu mbio za uhuru mwaka huu
nchini,Dkt Mukangara amewataja wajumbe hao kuwa ni Mkuu wa mkoa wa Dar
es Salaam, Said Meck Sadiq (Mwenyekiti) na Wajumbe wengine
katika kamati hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, Mkurugenzi
wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, Naibu Mkurugenzi wa Michezo
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda
na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa. Wengine ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu Mhariri
Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), Gabriel Nderumaki, George
Kavishe kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa Uhuru,
Jossiah Mfungo na Habib Gunze wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Mratibu
wa mbio za uhuru nchini Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa
habari juu ya mipango mbalimbali ya mbio za uhuru nchini ,Kulia ni
Waziri wa habari,Vijana,utamaduni na michezo Dr Fenella Mukangara ambapo
waziri amewateuwa wajumbe kumi watakaoratibu mbio hizo mwaka huu.
Baadhi
ya waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali nchini wakiwa katika
chumba cha mikutano cha wizara ya habari tayari kumsikiliza Mheshimiwa
waziri atangaze kamati hiyo.
***********
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara jana
alitangaza wajumbe watakaosimamia mbio za Uhuru Marathon ambazo
zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Dk. Fenella alisema wajumbe wa kamati hiyo itakayokuwa na watu 10 itakuwa na jukumu la kuhakikisha mbio hizo zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kamati
hiyo inatarajiwa kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiq huku ikiwa na wajumbe wengine kutoka katika sekta mbalimbali
nchini.
Wajumbe
wengine katika kamati hiyo iliyoundwa na waziri ni Mkuu wa Wilaya ya
Temeke, Sofia Mjema, Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan
Kijazi, Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda na Mkurugenzi msaidizi Idara ya
Habari, Zamaradi Kawawa.
Wengine
ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), Gabriel Nderumaki,
George Kavishe kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa
Uhuru, Jossiah Mfungo na Habib Gunze WA Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania.
Waziri
Fenella alisema mbio hizo zitakuwa zimegawanyika katika sehemu nne
kukiwa na mbio ndefu za kilomita 42, mbio za kati kilomita 21, mbio za
kujifurahisha kilomita 5 na mbio fupi ambazo ni maalumu kwa viongozi
zikiwa za kilomita 3.
“Mbio
hizi zina lengo kuu la kuimarisha umoja, upendo, mshikamano na amani kwa
Taifa letu. Tunategemea Watanzania wengi, ikiwa pamoja na viongozi
mbalimbali wa Serikali, dini, wanafunzi wa ngazi mbalimbalio na wananchi
kwa ujumla wataungana na kushiriki mbio hizi,” alisema.
Naye
Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema wazo kubwa la
kuanzisha mbio hizo ilikuwa ni kutaka kuwakumbusha Watanzania kuuenzi
umoja, amani, mshikamano ulipo pamoja na uhuru wetu.
Mratibu
huyo alisema, mpaka sasa wanariadha zaidi ya 300 kutoka nje ya Tanzania
wameomba kushiriki mbio hizo za aina yake hapa nchini.
“Sisi
kama vijana tukaona kuna haja ya kufanya kitu cha kuwakumbusha
Watanzania wenzetu kwani tunatakiwa kudumisha urithi wa amani,
mshikamano na uhuru wetu tulioachiwa na mababu zetu,” alisema.
Melleck
alisema mbali na mbio hizo kufanyika siku hiyo, pia kutakuwa na tamasha
kubwa la burudani litakalofanyika katika Viwanja vya Leaders vilivyopo
Kinondoni, Dar es Salaam ikiwa ni mkesha wa kusubiri siku ya Uhuru.
Mbali
na hayo Waziri Fenella naye alizitaka taasisi mbalimbali kuhakikisha
wanazidhamini mbio hizo kwani zina manufaa kiubwa kwa taifa.
No comments:
Post a Comment