Owen anasema Liverpool hawana njia mbadala isikuwa ni kuchukua mpunga wa Suarez pichani juu.
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Michael Owen anaamini kuwa Liverpool hawana njia mbadala ya kufanya isipokuwa kuchukua fedha na kuachana na mshambuliaji anayetaka kuondoka ndani ya klabu hiyo Luis Suarez.
Mshambuliaji huyo raia wa Uruguay ambaye tayari ameshakuwa akihusishwa na kutaka kuelekea Arsenl ambako inaarifiwa kuwa ofa mbili zimekataliwa na klabu yake, usiku wa jana aliweka wazi kupitia mahaojiano yake na magazeti kuwa anataka kuondoka Anfield.
Owen alijiunga na Real Madrid akitokea Liverpool kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £8 mwaka 2004 kufuatia hali ya sintofahamu ndani ya Merseyside na klabu yake kuamua kumuuza.
Alipoulizwa kama Liverpool nini inatakiwa kufanya alijibu: ‘Ni bahati mbaya jibu lake ni ndiyo.
‘Ni ushindi kwa mchezaji kutumia nguvu na kama una mchezaji ambaye hana raha na ni rasilimali hutakuwa na lingine la kufanya kuchukua pesa tu.
‘Si kama zamani unaweza kuwa naye katika benchi na kwa ujira mdogo na kumfanya ahangaike.
No comments:
Post a Comment