KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, September 12, 2013

Bei ya tiketi za soka yashuka Uingereza

Bei ya Tiketi za kutizama mechi za ligi kuu ya Uingereza zimeshuka kwa asilimia 2.4 kulingana na utafiti wa kitengo cha michezo cha BBC.
Utafiti huu uliojumuisha vilabu 166 kutoka kwenye daraja kumi bora nchini Uingereza,Imebaini kuwa kati ya msimu wa 2013 - 2014 bei ya kiingilio ya mechi ilishuka katika daraja nne za juu katika ligi ya Uingereza.
'' Hii ni Habari njema kwa mashabiki wa Kandanda ambao wamekuwa wakistahimili kupanda kwa bei mwaka nenda mwaka rudi '' Waziri wa michezo wa Uingereza Hugh Robertson aliiambia BBC.
''Vilabu vimebaini kuwa bei ya tiketi za kutizama mechi zimepanda kwa asilimia 11 ambayo ilikuwa ni mara nne ya kiwango cha mfumuko wa bei ya bidhaa asili.
Hilo limelazimu vilabu vianze kujali maslahi ya mashabiki wake kwa kupunguza bei.
Aidha idadi ya mashabiki wanaofika Viwanjani imeshuka kwa asili mia 5% ikiashiria mashabiki 9949 katika msimu wa mwaka wa 2011 -2012 hadi mashabiki 9481 katika msimu wa 2012-2013.
Mashabiki walilazimika kutoa takriban pauni 336.23 kutizama mechi zote katika msimu asilimia 2.4 chini ya msimu uliokwisha ambapo tikiti za msimu ziligharimu pauni 344.63 .
Tiketi ghali zaidi katika ligi ya premia ni ile ya Arsenal ambayo inagharimu pauni 126 katika eneo maalum na pauni 26 katika maeneo ya kawaida.
Aidha tikiti nafuu zaidi ya msimu ni ile ya Manchester City ambayo inauzwa kwa pauni 299 pekee huku ile ya Arsenal ikiorodheshwa kuwa ghali mno ikiuzwa kwa pauni 1,955.
Na ukitaka kikombe cha chai kuwa tayari kutoa pauni 2.50 ukiwa old Trafford nyumbani kwa Manchester United.

No comments:

Post a Comment