Picha za uwanja ambao Qatar wanataka kuanda michuano ya 2022 |
Kamati andalizi ya Kombe la dunia la mwaka wa 2022
itakayokuwa Qatar imekatalia mbali pendekezo la shirikisho la soka
duniani FIFA ya kupeana mashindano hayo kwa taifa lingine.
FIFA imependekeza kuhamisha kidumbwedumbwe hicho
hadi msimu wa baridi ili kuepuka viwango vya juu vya joto kama inavyo
shuhudiwa katika mataifa ya Ghuba.
Viwango vya joto huwa vinapanda hadi nyuzi joto 40 C.
Mwenyekiti wa shirikisho la soka la Uingereza
Greg Dyke amesema iwapo hakutakuwa na makubaliano ya kubadilisha saa za
kuandaa mechi za kombe la dunia basi hakutakuwa budi ila kubadili
uwenyeji wa kombe la dunia.
Hata hivyo Katibu wa kamati andalizi ya
mashindano hayo ya QATAR 2022 Hassan al Thawadi amekatalia mbali hoja
hiyo akisisitiza Qatar ilishinda fursa hiyo ya kuandaa kombe la dunia la
mwaka 2022 na ni sharti watimize azma yao.
''Tulijitahidi kunadi muundo msingi wetu na
tukafaulu kuwa mwenyeji wa kombe la dunia tukizingatia sera na mifumo ya
FIFA itakuwaje sasa inasemekana kuwa tulikosea ''
Mwenyekiti huyo alifoka baada ya Rais wa FIFA
Sepp Blatter Kuduwaza ulimwengu kwa kukukiri kuwa Shirikisho la FIFA
Lilikosea kuteua Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka wa 2022.
Qatar ilizipiku Korea Kusini, Japan Australia na Marekani iliposhinda uwenyeji wa mashindano hayo .
No comments:
Post a Comment