KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, September 13, 2013

Cape Verde yaadhibiwa na FIFA na kuondolewa katika kinyanganyiro cha kufuzu kombe la dunia.

Kikosi cha Cape Verde hakitashiriki mchuano wa kombe la dunia mwaka 2014
Cape Verde imebanduliwa nje ya kinyanganyiro cha kufuzu kwa kombe la dunia mwakani kwa nchi za Afrika.

Kwa mujibu wa tovuti ya shirikisho la soka duniani FIFA, Cape Verde ilikosea kwa kumtumia mchezaji aliyekuwa amepigwa marufuku katika mechi yao dhidi ya Tunisia Jumamosi iliyopita.

Kwa mujibu wa FIFA Fernando Verela hakustahili kucheza katika mechi hiyo waliyoshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Tunisia. 

FIFA sasa imebadilisha matokeo hayo na kuipa Tunisia ushindi mkubwa wa mabao 3-0 .

Kundi B
Tunisia - 14
Cape Verde - 9
Sierra Leone - 8
Eq Guinea - 2
Hatua hiyo imeipa Tunisia alama za kutosha kuipiku Cape Verde kutoka kileleni mwa kundi B ikiwa na alama 14.Cape Verde ni ya pili na alama 14.

Shirikisho la soka la Cape Verde lilimetozwa faini ya dola $ 6400.
 Cape Verde ilinufaika na alama za bwerere mapema mwaka huu pale Equatorial Guinea ilipoadhibiwa kwa kumtumia mchezaji kinyume na sheria za FIFA za uraia wa wachezaji.

The Blue Sharks ya Visiwa vya Cape Verde walikuwa wamelazwa mabao 3-4 na Equatorial Guinea lakini FIFA ikabadilisha matokeo hayo kwani Emilio Nsue Lopez hakutimiza kanuni za uraiya wa taifa hilo .

Sasa Tunisia ndiyo itakayosonga mbele katika raundi ya mwisho itakayochezwa katika droo itakayofanyika Jumatatu tarehe 16.

No comments:

Post a Comment