Mchezaji anayeshikilia rekodi ya
dunia kwa kuwa mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa zaidi kusajiliwa
Gareth Bale, kesho atakuwa akishuka dimbani kwa mara ya kwanza kama
mchezaji wa Real Madrid pale itakapokuwa ikikabiliana na Villarreal, kocha wa
klabu hiyo Carlo Ancelotti amesema .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24
aliigharimu Real Madrid pauni milioni 85.3 kuhama kutoka kilabu ya
Tottenham ya Uingereza Septemba mosi
.
Bale hajarishiriki mechi yeyote
kikamilifu msimu huu kutokana na jeraha la mguu mbali na dakika 32
alizocheza Wales ilipolazwa 3-0 dhidi ya Serbia Jumanne.
Aidha kocha huyo Muitaliano amekiri atamtumia Bale kama mshambulizi wa upande wa kulia .
Bale kwa upande wake anasema angependa kuchangia
timu yake itakapokuwa ikitafuta ushindi wa nne katika mechi nne dhidi
ya Villarreal.
Kabla ya kununuliwa kwake Bale ,nyota wa zamani
wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo ndiye aliyekuwa
ameorodheshwa kama mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa zaidi duniani.
Ronaldo alinunuliwa kwa pauni milioni 80 kutoka Manchester United mwaka wa 2009.
No comments:
Post a Comment