Ghana itamenyana na Misri katika mechi za kuamua nchi
ya Afrika itakayowakilisha bara zima katika dimba la kombe la dunia
mwaka ujao nchini Brazil.
Misri kama nchi pakee ambayo imeshinda mechi
zake zote za makundi za kufuzu kushiriki kombe la dunia, bila shaka
imeitia hofu nchi zengine na bila shaka hakuna ambaye angependa
kukukutana nao.
Hii ni kutokana na matokeo ya draw
iliyofanywa ambapo mataifa ya kiafrika zitacheza kwenye michuano ya
kutafuta mwakilishi wa bara la Afrika Brazil mwaka ujao.
Mabingwa wa Afrika Nigeria watachuana na Ethiopia wakati Ivory Coast wakitoana jasho na Senegal.
Tunisia, waliofuzu baada ya Cape Verde watachuana na Cameroon.
Burkina Faso, nao waliomaliza wa pili katika michuano ya taifa bingwa Afrika watatoana jasho na Algeria.
Mechi za awamu ya kwanza ya michuano hiyo,
zitachezwa kati ya tarehe 11 na 15 Oktoba, huku mechi za marudio
zikichezwa kati ya tarehe 15-19 Novemba.
Shirikisho la soka duniani, Fifa, limezitaka
nchi hizo kuchagua tarehe za mechi, eneo wanalotaka kuchezea mechi yao
ya kwanza ifikapo Ijumaa wiki hii.
Wakati Ghana wanahisi kutokuwa na bahati baada
ya kuamuliwa kuwa watacheza na Misri, wanaweza kujipa moyo kwani
waliwahi kuwashinda Misri kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Dubai
mwezi Januari.
Na haijulikani ikiwa Misri watacheza mechi yao ya marudio mjini Cairo kwani mgogoro wa kisiasa unatokota nchini humo.
No comments:
Post a Comment