KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 3, 2012

RWANDA KUMBE ILIJITABIRIA KUFUNGWA NA KILIMANJARO STARS.

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Rwanda(Amavubi) Erick Nshimiyimana.
 Wakati timu ya ya taifa ya Rwanda ikifungasha virago na kurejea nyumbani katika jiji la Kigali baada ya kuondoshwa katika michuano ya kombe la Kagame na Kilimanjaro Stars kwa kufungwa mabao 2-0, kocha msaidizi wa timu hiyo maarufu kama Amavubi) Erick Nshimiyimana alijitabiria kufungwa na Kilimanjaro Stars.
 
Baada ya mchezo wa kwanza wa Kilimanjaro wa hatua ya makundi ambapo ilianza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudani mchezo uliochezwa katika uwanja wa Namboole, Nshimiyimana alikaririwa akisema wazi kuwa ameiangalia kwa makini timu hiyo na kusema Kilimanjaro haikamatiki.
 
Alikaririwa akimuuliza kwa mshangao mwandishi wa habari hii,
"Hivi huyu kocha ana muda gani?(mwandishi wa habari hii alimjibu kuwa hata mwaka hajafikisha tangu alipokabidhiwa timu ndipo alipoendelea kusema.
"Hii timu imebadilika sana kama itaendelea kucheza hivi hakuna ubishi kwamba itafika mbali na huenda ikachukua hata ubingwa,".alisema Nshimiyimana.

Nshimiyimana ambaye pia ni kocha wa timu ya APR  ya Rwanda amesema, Kilimanjaro Stars imekamilika kila idara kuanzia ufundi hadi fiziki ya wachezaji.
 
"Nimewaangalia kwenye fiziki na hata mbinu wako vizuri na hata wanapotengeneza mashambulizi unaona kabisa yamepangiliwa,"
 
Timu ya taifa ya Rwanda hii leo imeyaaga mashindano ya kombe la chalenji baada ya kupokea kipigo toka kwa timu ya taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars cha mabao 2-0 yaliyofungwa na kiungo Amri Kiemba na John Bocco.

Ushindi huo unaifanya Kilimanjaro kusubiri mshindi wa mchezo wa robo fainali nyingine baina ya wenyeji Uganda dhidi ya wawakilishi wa ukanda wa Afrika mashariki na kati katika michuano ya mataifa ya Afrika Ethiopia mchezo ambao upapigwa hapo kesho Namboole.

No comments:

Post a Comment