Cristiano Ronaldo amesema kuwa anataka kusalia kuwa
Real Madrid kama mchezaji soka baada ya kutia saini mkataba mpya na
mabingwa wa ligi ya Uhispania hadi mwaka 2018.
Ronaldo ambaye ni mchezaji muhimu wa timu yake
ya taifa ya Ureno, awali ilisemekana alikuwa anaelekea Machester United
kilabu yake ya zamani.
"Manchester United imepitwa na
wakati, nyumbani kwangu sasa ni Real Madrid," alisema Ronaldo. "natumai
nitasalia hapa hadi nitakapostaafu kucheza. Hii ndio kilabu bora zaidi
duniani, aliongeza kusema Ronaldo.
Ronaldo atakuwa analipwa pauni milioni 14.25 kila mwaka.
Mkataba wake Bernabeu ulikuwa unakamilika mwaka 2015.
Ronaldo alijiunga na Real kutoka Ligi ya Uingereza mwaka 2009 kwa kima cha zaidi ya dola milioni themanini.
Ameingiza mabao 203 katika mechi 203 akichezea
Los Blancos, na kuwasaidia kushinda La Liga kati ya mwaka 2011-12 pamoja
na kupata mataji mawili ya nyumbani.
Ronaldo aliteuliwa wa pili nyuma ya Lionel Messi katika shindano la mchezaji bora duniani mwaka 2011 na 2012.
Lakini baadhi wamehoji mustakabali wa mwanasoka huyo hasa baada ya Real kumnunua Gareth Bale kutoka Tottenham.
Pamoja na kutaka kuhamia Man U, Ronaldo alihusishwa na kilabu ya Monaco.
"nina heshimu vilabu vyote ambavyo huniulizia
lakini daima wanajua kuwa mimi nataka kuendelea kucheza hapa Real, hadi
nitakapostaafu kutoka Soka.'' alinukuliwa akisema Ronaldo
No comments:
Post a Comment