KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 23, 2013

Kufukuzwa kwa Paolo Di Canio, Sam Allardyce anasema ni maamuzi ya haraka yasikuwa na fikra.

Bosi wa West Ham Sam Allardyce anaamini kuwa maamuzi wa Sunderland kumfuta kazi meneja wake Paolo Di Canio ni ya kukurupuka yasiyofuata fikra za kina.
Mtaliano Di Canio, mwenye umri wa miaka 45, aliondolewa kazini Jumapili baada ya michezo mitano tu ya msimu huu wa ligi kuu ya England
Bosi huyo wa zamani wa Swindon aliaajiriwa mwezi Machi kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Martin O'Neill.

Safari ya Di Canio

  • Alizaliwa Rome, Julai 9 mwaka 1968
  • Amechezea vilabu vya  Lazio, Juventus, Napoli, AC Milan, Cisco Roma
  • Akicheza Uingereza katika vilabu vya Celtic, Sheffield Wednesday, West Ham na Charlton
  • Alipigwa faini na FA ya pauni milioni £10,000 mwaka 1998 baada ya kumsukuma mpaka chini mwamuzi Paul Alcock baada ya kumta  nje ya uwanja katika mchezo dhidi ya Arsenal
  • Alishinda tuzo ya Fifa ya Fair Play mwaka 2001 kwa kusimamisha mpira ili kuruhusu mlinda mlango wa Everton Paul Gerrard apewe matibabu.
  • Amekosolewa mwaka 2005 kwa mtindo wake wa kuukumbatia mfumo wa Ki-fashist kwa kupiga saluti katika mchezo dhidi ya Lazio.
  • Aliaajiriwa kuwa bosi wa Swindon mwezi Mei 2011 na kuiongoza mpaka kucheza League One mwaka uliofuata
  • Alijiuzulu ubosi Swindon mwezi February 2013 kwa kwenda kwenda kinyume na klabu kwa kumuuza nyota Matt Ritchie
  • Alichukua nafasi ya Martin O'Neill kama bosi wa Sunderland mqwezi March 2013 wakati klabu hiyo ikijaribu kujinasua na hatari ya kushuka daraja.
  • Amefukuzwa kazi baada ya kufungwa michezo minne kati ya michezo mitano ya ligi ya msimu wa  2013-14
"Endapo mambo hayaendi vizuri basi ni kama watakuwa wanafanya maamuzi yasikuwa na fikra za kina kama wanataka kubadili meneja,"Amesema Allardyce, ambaye aliondoka kazini Newcastle mwaka 2008 baada ya miezi minane kwa hiari yake mwenyewe.
Hakuna meneja hata mmoja kati ya hawa wanne wa Sunderland Ricky Sbragia, Steve Bruce, O'Neill na Di Canio, waliomaliza michezo 100 jambo ambalo Allardyce atakuwa akikamilisha katika akiwa West Ham hapo kesho watakapokuwa wakikabiliana dhidi ya Cardiff.

No comments:

Post a Comment