KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, October 24, 2013

Mwamuzi wa mechi ya City hafai

Mwamuzi aliyesimamia mechi ya Manchester City dhidi ya CSKA Moscow hafai tena kuchezesha mechi yoyote, kwa kushindwa kuzuia matukio ya ubaguzi wa rangi uwanjani.
Toure anadai mashabiki walimtukana kwa kutumia matamshi ya ubaguzi wa rangi
Hayo ni maoni ya mwenyekiti wa chama cha kuzuia ubaguzi wa rangi katika soka nchini Uingereza, Kick It Out, Lord Ouseley.
Mchezaji wa Manchester City, Yaya Toure, alikuwa amemlalamikia refa Ovidiu Hateganabout, kufuatia kelele za ubaguzi wa rangi kutoka kwa mashabiki wa CSKA katika mechi yao ya ligi ya klabu bingwa Ulaya, na ambayo City ilipata ushindi.
"Huyu mwamuzi hafai kuchezesha tena mechi," aliielezea BBC.
"Alishindwa kutekeleza wajibu wake usiku wa jana, na hili ni suala wazi ambalo Uefa inafaa kupambana nalo."
Kufuatia muongozo ambao ulitolewa na shirikisho la kusimamia soka la Ulaya, Uefa, mwaka 2009, waamuzi wana mamlaka ya kusitisha matamshi ya ubaguzi wa rangi uwanjani kutoka kwa mashabiki.
Mwamuzi, kama hatua ya kwanza, anaweza kusitisha mchezo, na kuamuru kutumia vipaaza sauti uwanjani katika kuwaonya mashabiki.
Kati ya hatua ambazo zimetekelezwa na Uefa dhidi ya vilabu vilivyohusika katika matukio ya ubaguzi wa rangi ni pamoja na kuwafungia mashabiki viwanja vya Dinamo Zagreb ya Croatia, Legia Warsaw ya Poland na Honved ya Hungary.
Uwanja wa Lazio pia ulikuwa umefungwa kabisa, lakini baada ya kukata rufaa, kwa kiasi fulani mashabiki waliruhusiwa tena.
Viwanja ambavyo bado havijafunguliwa kikamilifu kwa mashabiki ni vile vya Poland, Lech Poznan na Piast Gliwice, na vile vya APOEL Nicosia ya Cyprus na HNK Rijeka ya Croatia.
Hatua ya pili ya mwamuzi ni kuusimamisha mchezo kwa muda, na rabsha za ubaguzi wa rangi zikiendelea, kuisimamisha mechi kabisa.
Kwa kuwa Toure aliripoti matukio hayo kwa mwamuzi wakati wa mechi, na pia kuzungumza naye baadaye, tukio hilo litaandikishwa katika ripoti rasmi ya mechi, na kufikishwa Alhamisi kwa Uefa.
Manchester City, kama klabu, pia imewasilisha malalamiko hayo kwa Uefa.
Hata hivyo, mwandishi wa BBC mjini Moscow, Steve Rosenberg, anasema klabu ya CSKA Moscow inadai kwamba Toure peke yake ndiye alizisikia kelele hizo za ubaguzi wa rangi.

No comments:

Post a Comment