Ushindi wa Super Eagles ya Nigeria ugenini dhidi ya Ethiopia umeipa matumaini ya kushiriki kombe lijalo la dunia.
Ethiopia ilipata goli la kuongoza kunako dakika ya 56 kupitia mchezaji Asefa.
Bao hilo halikukaa kwa muda mrefu.kunako dakika ya 67 mkwaju uliopigwa na Emanuel Emenike uliishia langoni na kuwa 1-1.
Ethiopia watajilaumu wenyewe kwa kushindwa
kutumia nafasi kadhaa walizopata na pengine waliponea chupuchupu kunako
dakika 77 ambapo mkwaju wa Nigeria ulirudishwa na mlingoti wa lango.
Goli la ushindi la Nigeria limepatikana kwenye
dakika ya mwisho kwa njia ya penalty iliyofungwa kimiani na Emmanuel
Emenike na kupalilia njia kwa bingwa hao wa Afrika ya kwenda Brazil.
No comments:
Post a Comment