Cristiano Ronaldo anapokuwa nje ya uwanja anakuwa mbali na kuonyesha vazi lake la ndani, lakini Ronaldo ambaye ni mtulivu kitabia ameonekana kuonyesha mwili wake kwa kuzindua vazi jipya la ndani(chupi).
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United amejiunga na wabunifu wa mavazi kwa kubuni vazi hilo ambalo litakwenda sokoni kwa jina lake wiki hii.
Taarifa njema ni kuwa sehemu ya faida ya mauzo ya vazi hilo litakwenda kwenye msaada huku Ronaldo kwa lengo la kurejesha kwenye jamii.
Anaungana na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Galatasaray Didier Drogba huku Drogba ambaye naye atakuwa na vazi kama hivo lililotengenezwa kwa rangi za machungwa na kijani.
No comments:
Post a Comment