Polisi jijini Dar es Salaam Tanzania wamelazimika
kutumia Mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki wa Klabu ya Simba, baada
ya kumalizika mechi ya Ligi kuu soka Tanzania bara hii leo kwa matokeo ya sare baina ya Simba na Kagera Sugar.
Vurugu hizo zimezuka mwishoni mwa mechi ambayo
timu ya Simba imezidi kuporomoka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa
ligi hiyo kufuatia matokeo ya sare ya bao 1-1.
Baada ya Simba kuongoza bao 1 hadi
dakika ya 90 Kagera Sugar walisawazisha kwa Penati iliyotiwa kimiani
na beki wa zamani wa Simba Salum Kanoni ambapo mashabiki wanaoaminika
kuwa wa Simba walianza kung'oa viti uwanjani hali iliyosababisha askari
polisi kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya mashabiki hao.
Simba ilianza kuliona lango la Kagera Sugar
katika dakika ya 45 baada ya mshambuliaji raia wa Burundi Amis Tambwe
kufunga bao la kwanza lililodumu hadi mapumziko.
Katika Kipindi cha pili Simba walianza kucheza
kwa kujihami hali iliyosababishga Kagera kukaribia lango lao mara kwa
mara na hatimaye wakafanikiwa kusawazisha katika dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo Simba imeporomoka hadi nafasi
ya nne wakiwa na pointi 21,huku Azam, wakishika nafasi ya kwanza kwa
kuwa na pointi 23 sawa na Mbeya City lakini wakitofautiana kwa magoli ya
kufunga.
Yanga ni ya tatu kwa kuwa na pointi 22.
No comments:
Post a Comment