Mchezaji maarufu wa Kriketi nchini India Sachin
Tendulkar ametangaza atastaafu kutoka katika mchezo huo baada ya kucheza
kwa mara ya 200 mwezi ujao.
Tendulkar mwenye umri wa miaka 40 na kinara wa
zamani wa timu wa India , aliyestaafu kutoka kwa mchuano wa siku moja wa
kimataifa mwaka 2012, atastaafu baada ya kucheza mechi mbili dhidi ya
West Indies.
"ni vigumu kutafakari maisha bila
kucheza Kriketi, kwa sababu ndio nimekuwa nikifanya tangu nikiwa miaka
11,'' alisema Tendulkar.
Tendulkar ndiye mchezaji aliyeweza kuwa na
mikimbio mingi zaidi kuliko wote ikiwa 15,837 katika michuano 198 ya
mataifa yenye hadhi ya juu au Tests na mikimbio mingine 18,426 katika
michuano mingine 463 ya ODIs.
Alianza kucheza kimataifa akiwa na umri wa
miaka16 mwezi Novemba mwaka 1989 na mwaka jana akawa mchezaji pekee
katika historia ya mchezo huo kufikisha senchari 100.
"Maisha yangu yote nimekuwa nikiota kuhusu
kucheza kriketi India. Na nimekuwa nikiishi katika ndoto hii kwa miaka
24 iliyopita,'' alisema.
Tendulkar alicheza mchezo wake wa mwisho wa
michuano ishirini kati ya timu yake ya Mumbai na Rajasthan Royals
inayoongozwa na skipa wa zamani wa India na mchezaji mwenzake Rahul
Dravid.
Tendulkar atacheza katika mechi yake ya mwisho
kitaifa nchini India na amesema kuwa litakuwa jambo la heshima sana
kwake kuwakilisha nchi yake kote duniani.
No comments:
Post a Comment