MBUNGE wa Handeni Dkt Abdallah Kigoda, ameaahidi kushirikiana na
kuwasaidia waandaaji wa Tamasha la Utamaduni na Michezo lililopewa jina la
‘Handeni Kwetu’ litakalofanyika Desemba 14 mwaka huu mjini Handeni, mkoani
Tanga, ili kuunga mkono jitihada za wadau katika suala zima la utamaduni na
maendeleo.
Akizungumza
wakati akizindua kisima cha maji katika soko la zamani lililopo katika mji wa
Chanika, Dkt Kigoda, alisema anaunga mkono tamasha hilo ambalo litaibua fikra
na mtizamo mpya wa utamaduni miongoni mwa wananchi wilayani hapa.
“Waandaji wa
Tamasha la Utamaduni wamenipa taarifa za kufanyika tamasha hilo nami kama
mbunge wa jimbo hili sina budi kuwaunga mkono kufanikisha tamasha hilo na
nitashirikiana nao,” alisema Dkt Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda,
Biashara na Masoko.
Dkt Kigoda
alisema suala la utamaduni ni suala mtambuka ambalo linagusa mioyo ya wananchi
wengi hivyo unapoweka tamasha kwa ajili ya utamaduni wa ngoma licha ya kuwapa
burudani wananchi hutoa hamasa kwa vijana kupenda mila na utamaduni hasa suala
na ngoma za asili.
Mbunge huyo
alitoa wito kwa wananchi wilayani humo na wale waliopo nje ya handeni
kujitokeza kushiriki tamasha hilo ili kuibua mawazo mapya juu ya masuala ya
utamaduni na michezo yaliyokosa msisiko kutokana na kutopewa kipaumbele.
Mbunge huyo,
aliahidi kusaidia tamasha hilo baada ya kupewa taarifa na mwandaaji wake Kambi
Mbwana.
Wadhamini
waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Phed Trans
inayomilikiwa na Yusuphed Mhandeni, Grace Products, Screen Masters, Dullah
Tiles $ Construction Ltd, Katomu Solar Specialist na Country Business Directory
(CBD) na Michuzi Media Group.
Wengine
ni duka la mavazi la Chichi Local Ware, SmartMind & Partners chini ya ANESA
COMPANY LIMITED, ikidhamini kwa kupitia kitabu cha ‘NI WAKATI WAKO WA KUNG'AA,
Screen Masters, Saluti5.com, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa
Letu Blog.
Katika hatua
nyingine, mbunge huyo alisema kuwa wataalamu wanafanya utafiti kwa ajili ya
kuchimba kisima katika uwanja wa mpira wa Azimio ambao unakarabatiwa ili uweze
kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu na klabu ya Mgambo JKT.
Alisema
tayari ametoa kiasi cha shilingi milioni 250 kutoka katika mfuko wake wa
maendeleo ya jimbo ili kuukarabati uwanja huo ambao tayari umeoteshwa nyasi
mpya na kujengwa vyumba vya kubadilishia ngu wachezaji pamoja na jukwaa kuu.
No comments:
Post a Comment