KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, November 14, 2013

Frank Ribery:Nitashinda tuzo ya Ballon d'Or na kuwapiku Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

 Mshambuliaji wa  Bayern Munich Frank Ribery amesema anastahili kushinda tuzo ya Ballon d'Or zaidi ya wapinzani wake Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Mfaransa huyo ameng'ara mwaka huu wa 2013 ndani ya kikosi cha Bavarians ambapo amechochea ushindi wa taji wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, ushindi wa taji wa DFB-Pokal pamoja na ushindi wa taji la vilabu bingwa Ulaya, na sasa akiwa chini ya kocha mpya ndani ya msimu hii Pep Guardiola ameanza kwa mtindo ule ule wa kutisha pia.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani atakuwa na kazi kubwa ya kuwashinda mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi na mwingine wa Real Madrid Ronaldo, ,lakini anaonekana kujiamini zaidi kwa kuwa na maendeleo mazuri ya ndani ya kipindi cha miezi 12 iliyopita.

"Najaribu kupotezea tuzo ya Ballon d'Or, lakini mke wangu tayari ameshaandaa sehemu ya kutunza tuzo hiyo juu ya fireplace sebuleni.

"Before I was a good player, now I think I'm the best."


Ribery anatarajiwa kuwepo katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa itakayocheza mchezo wa mtoano kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia dhidi ya Ukraine wiki ijayo wakiaanzia ugenini Ijumaa.

No comments:

Post a Comment