KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, November 14, 2013

Gerard Pique: Nitafurahi Messi akishinda Ballon d'Or kwa mara ya tano.

Mlinzi wa Barcelona Gerard Pique amedai kuwa atafurahi sana kama mchezaji mwenzake Lionel Messi akishinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mara ya tano mfululizo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa katika maumivu ambayo si rahisi kumfanya kushindwa na akina Cristiano Ronaldo na Franck Ribery ambao ndio washindani wake wakubwa katika kinyanganyiro hicho.

Mlinzi huyo wa kati wa zamani wa Manchester United anaamini kuwa Messi bado ni miongoni mwa wachezaji wenye kupewa nafasi kubwa kutokana na umaarufu wake.

Akiongea na Mundo Deportivo mlinzi huyo amesema
"Leo hawezi kutolewa. Huu ni ushindani ambapo watu wanapiga kura. Alishinda mara nne na alikubalika kwa watu"

"Endapo atashinda nitafurahi sana. Mimi ni shabiki mkubwa wa Leo, siku zote nimekuwa nikisema hilo. Kama tutamchambua kwa mwaka huu, alikuwa na kipindi kizuri tena.

No comments:

Post a Comment