Middlesbrough imemtaja meneja msaidizi wa zamani wa Real Madrid Aitor
Karanka kama mkuu mpya wa benchi la ufundi kwa mkataba ambao utamalizika 2016.
Karanka mwenye umri wa miaka 40, aliwahi kufanya kazi chini ya Jose Mourinho kwa miaka mitatu ndani ya viunga vya Bernabeu, lakini hajawa bado na uzoefu wa kama meneja.
Mlinzi huyo wa zamani wa Real na Hispania aliondoka kwa mabingwa hao mata tisa wa Ulaya wakati Carlo Ancelotti alipochukua urithi wa kuiongoza timu hiyo kutoka kwa Mourinho kama maneja wakati wa kiangazi.
Karanka ni nani?
- Alizaliwa Vitoria, nchini Hispania mwaka 1973
- Akiwa kama mlinzi alifanikiwa kuichezea Hispania mchezo mmoja na kabla ya hapo alikuwa akiichezea Athletic Bilbao na Real Madrid akichezea pia Colorado Rapids
- Amekuwa msaidizi wa Jose Mourinho viungani Bernabeu kuanzia 2010 mpaka 2013
Anakuwa bosi wa kwanza wa Middlesbrough kutoka nje ya England.
Amenukuliwa akisema
"Ni muda wangu na najua niko tayari. Nimefanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu na Jose na alikuwa akisaidia kila siku na nimejifunza sana.
"Nimezungumza naye na amenitaka nije hapa ana niamini sana katika hili."
Meneja wa zamani wa klabu hiyo Tony Mowbray aliiacha klabu hiyo kutoka pande za Riverside mwezi uliopita na tangu wakati huo msaidizi wake Mark Venus amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda.
Kwasasa Middlesbrough wako katika nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi ndogo ya pili kwa ukubwa nchini England ya Championship.
Itakumbukwa miaka saba iliyopita Middlesbrough ilifikia fainali ya Uefa Cup
kabla ya kupoteza kwa Sevilla mchezo uliokuwa wa mwisho wa Steve McClaren kabla ya kupindukia katika umeneja.
.
No comments:
Post a Comment