Roma imekuwa timu ya kwanza kushinda michezo yote 10 ya mwanzo wa ligi ndani ya msimu wa Serie A baada ya kuichapa Chievo 1-0 hapo jana.
Goli la kwanza ndani ya msimu huu kutoka kwa mshambuliaji Marco Borriello lilitosha kuwapa vinara hao wa msimamo wa ligi ya Italia wakiwa katika uwanja wa nyumbani dhidi ya washika mkia katika msimamo Chievo.
Roma, ambao wamefunga jumla ya magoli 24 na kuruhusu goli moja msimu huu mpaka sasa wanaongoza kwa tofauti ya alama tano dhidi ya wanaoshika nafasi ya pili Napoli.
Amenukuliwa mfungaji wa bao hilo Borrielo akisema
"Ni mafanikio mazuri tuliyofanya katika historia lakini tunapaswa kuangalia mbele tuendako tunamchezo na Torino," .
"Pia tumecheza vizuri ugenini lakini lengo letu ni kufuzu vilabu bingwa Ulaya."
Rekodi ya ushindi msimu huu
25 Aug: Livorno (away) 2-001 Sep: Verona (home) 3-0
16 Sep: Parma (away) 3-1
22 Sep: Lazio (home) 2-0
25 Sep: Sampdoria (away) 2-0
29 Sep: Bologna (home) 5-0
05 Oct: Inter Milan (away) 3-0
18 Oct: Napoli (home) 2-0
27 Oct : Udinese (away) 1-0
31 Oct: Chievo (home) 1-0
Kikosi cha Rudi Garcia kiliweka rekodi ya kushinda michezo tisa iliyokuwa ikishikiliwa na Juventus mwishini mwa wiki huku shukrani ikiwa ni kwa goli la dakika za mwisho katika mchezo dhidi ya Udinese ambapo walishinda bao 1-0.
Juve waliweka rekodi hiyo katika msimu wa 2005-2006,
ambapo kigogo hicho cha Turin kilivuliwa ubingwa kutokana na kashfa ya upangaji wa matokeo.
Licha ya kumosa nahodha wake Francesco Totti na Gervinho
ambao ni majeruhi na mlinzi Douglas Maicon kusimamishwa, bado Roma
walitawala mchezo lakiwa walishindwa kupata bao katika kipindi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment