|
Jeshi la polisi limelazimika kutumia nguvu kwa kurusha hewani mabomu ya kutoa machozi kwa lengo la kutuliza vuruvu uwanja wa taifa baada ya mchezo wa soka wa ligi kuu ya Tanzania bara baina ya Simba na Kagera Sugar hasa baada ya Kagera kupata bao la kusawazisha lililofungwa kwa njia ya penati na Salumu Kanoni. |
|
Kitendo cha kung'oa viti kinetokea wakati ambapo wapenzi wa soka bado wana kumbukumbu ya rai ya mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi wa uwanja huo tarehe 15 Februari 2009 ambapo aliwataka watanzania kuutunza uwanja huo kwani ni uwanja mzuri ambao umejengwa kwa gharama kubwa kwa kutmia kodi za watanzania wenyewe kwa kushirikiana na watu wa China.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida hii leo watanzania wachache wamesahau walikotoka na kuanza kuuharibu uwanja huo kwa hasira za kuazima kwa muda bila ya kujifahamu kuwa wanachofanya ni kuwakosea watanzania walio wengi wenye uchungu na kodi zao.
|
Rais Hu Jintao wa China akiambatana na rais Jakaya Kikwete wa
Tanzania tarehe 15 walihudhuria uzinduzi wa uwanja mpya wa michezo wa
taifa wa Tanzania uliojengwa kwa msaada wa China. Kwenye sherehe hiyo, rais Kikwete akiwaongoza Watanzania zaidi ya elfu 6 waliwapokea wageni kutoka China kwa ukarimu mkubwa.
Uwanja huo wa michezo ni mradi mkubwa zaidi uliosaidiwa na China
baada ya ujenzi wa reli ya TAZARA.
Huu ni uwanja wa kisasa wenye uwezo
wa kuchukua watazamaji elfu 60, na una vifaa vya kisasa kutosha kuandaa
michezo mikubwa ya ngazi ya bara, na mashindano mbalimbali ya shirikisho
la soka la kimataifa na shirikisho la riadha la kimataifa.
Ujenzi wa
uwanja huo ulianza mwezi Januari mwaka 2005, na kukamilika mwezi
Februari mwaka 2008. Hivi sasa huu ni uwanja mkubwa zaidi na wa kisasa
zaidi barani Afrika.
Rai yangu watanzania wenzangu na wapenda soka kama ni vurugu za upenzi kwa timu zenu zifanyike nje ya uwanja na si ndani tena kwa kuvunja na kungoa viti vya uwanja huo.
Kama tumeshindwa kujizuia na kuendeleza ustarabu uwanjani vema turudi uwanja wa zamani maarufu kama SHAMBA LA BIBI tukabanane huko ambako nadhani wengi wetu tumeshasahau adhabu hiyo.
|
No comments:
Post a Comment