KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, October 31, 2013

FILIPPO INZAGHI ANASEMA HAKUNA MESSI WALA RONALDO ATAKAYEVUNJA REKODI YAKE. IPI HIYO SOMA......

 Mchezaji mkongwe wa AC Milan Filoppo Inzaghi amedai kuwa rekodi yake ya kufunga mabao katika michezo ya fainali ya michuano haikuwaja kufikiwa na mtu yoyote duniani hata awe Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Mshambuliaji huyo ambaye kwasasa ana umri wa miaka 40 alifunga jumla ya magoli nane katika michezo mbalimbali ya fainali wakati wa kipindi chake cha uchezaji soka ndani ya vilabu vyote vya Juventus na Milan.

Mkongwe huyo mtaliano anajivunia zaidi mwaka 2007 alifunga magoli mawili katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool mjini Athens, kabla ya kufunga magoli mengine mawili dhidi ya Sevilla na Boca Juniors katika michuano ya Uefa Super Cup na Fifa World Club Cup.

Inzaghi anamatumaini kuwa uwezo huo aliokuwa nao uwanjani hautakuja kufikiwa na mtu yoyote wakiwemo wachezaji wawili wanaofukuzana mara kwa mara katika kuwania tuzo ya Ballon d'Or.

"Kocha wetu kipingi kile Carlo Ancelotti alikuwa hana uhakika wa nani amtumie katika kati yangu na Alberto Gilardino katika fainali ya Athens, lakini alinipanga mimi na kufunga magoli yote mawili," alikuwa akiongea na La Gazzetta dello Sport.

"Tena nikafunga katika fainali ya Super Cup dhidi ya Sevilla and na bao lingine dhidi ya Boca Juniors.

"Magoli matano katika michezo mitatu ya fainali muhimu sana na kushinda michezo yote hilo ni jambo muhimu sana. Hakuna si Messi wala Ronaldo atafanikisha hilo. Ni rekodi nitabaki nayo."

No comments:

Post a Comment