KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 1, 2013

KLABU BINGWA AFRIKA: Ahly wanahaha kumponya mlinda mlango wao Ekramy kuelekea mchezo dhidi ya Pirates kesho.

Mabingwa Al Ahly ya Misri wanatoa jasho kupata ahueni kwa mlinda mlango wao Sherif Ekramy wakati ambapo Orlando Pirates wakiwa wametangaza wazi kuwa wako sawa kuelekea katika mchezo wa kwanza wa fainali ya vilabu bingwa barani Afrika hapo kesho mchezo ambao utapigwa katika kitongoji cha Soweto.
Uamuzi wa kama Ekramy atashiriki unatarajiwa kutolewa muda mfupi ujao kuelekea katika mchezo huo utakao pigwa uwanja wa Orlando hii ikiwa ni kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo ya kutoka katika jiji la Cairo.
Kumekuwepo pia na hali ya sintofahamu juu ya hali ya kiungo Hossam Ashour, ambaye amekuwa na matatizo ya bega.
Al Ahly ndiyo yenye rekodi ya juu ya kushinda taji la vilabu bingwa Afrika ikishinda mara saba huku Orlando Pirates ikishinda taji hilo mara moja.
Wachezaji wote hao wawili wamesafiri kuelekea Afrika kusini kwa ajili ya mchezo huo lakini wakifanya mazoezi mepesi tangu walipowasili kwa lengo la kujenga ubora wao taratibu.

Ekramy amekuwa katika majeraha tangu Misri ilipochapwa bao 6-1 na Ghana ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia mchezo uliopigwa katika mji wa Kumasi katikati ya mwezi uliopita.
Pirates inatarajiwa kumpumzisha kiungo wao mahiri Sifiso Myeni katika kikosi cha kwanza na wanatarajiwa kujaribu mshambuliaji raia wa Zambian Collins Mbesuma katika kikosi cha kwnaza tangu mwezi Agosti.

No comments:

Post a Comment