Kaimu katibu mkuu wa TFF Bonface Wambura Mgoyo. |
Wanachama
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wanatakiwa kufanyia
marekebisho katika katiba zao kwa kuingiza ibara ya Kamati za Maadili.
Maagizo
hayo yanatokana na kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF iliyoketi
Novemba 23 mwaka huu jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Rais
Jamal Malinzi ambapo pamoja na mambo mengine ilijadili umuhimu wa
wanachama wake kuunda kamati hizo.
Wanachama
wa TFF ambao muda wao wa uchaguzi umekaribia, wanatakiwa kufanya
marekebisho hayo kwanza kabla ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi.
TFF ina aina tatu za wanachama. Wanachama hao ni vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na Klabu za ligi Kuu.
No comments:
Post a Comment