Timu ya taifa ya Tanzania bara "Kilimanjaro Stars"
imesonga mbele hatua ya robo fainali ya mashindano ya Kombe la Mataifa
ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA Senior Challenge baada ya
kuisambatisha timu ya Taifa ya Burundi "Intamba mu Rugamba" kwa goli 1 - 0.
Goli la Tanzania limefungwa dakika ya 8 kipindi
cha kwanza na Mbwana Samatta mshambuliaji wa timu hiyo anachezea Klabu
ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kwa matokeo hayo ya mchezo huo wa kundi A
unaifanya Tanzania bara sasa kufikisha pointi 7 baada ya kushinda mechi
mbili na kutoka sare mmoja.
Tanzania ilitoka sare na Zambia ya goli 1 - 1
katika mchezo wa ufunguzi siku ya Alhamis iliyopita ambapo baadae
iliifunga Somalia goli 1 - 0 mechi iliyopigwa siku ya jumapili kabla ya
kushinda mechi kati yake na Burundi ya goli 1 - 0.
Katika mchezo mwingine wa kundi A Zambia walitarajiwa kupambana na Somalia.
No comments:
Post a Comment