KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, December 6, 2013

Kocha wa Tanzanite Rogasian Kaijage ana matumaini na kikosi dhidi ya Afrika kusini kesho.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya wanawake ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 'Tanzanite' Rogasian Kaijage amesema kikosi chake kiko vizuri kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Afrika Kusini (Basetsana) inayochezwa kesho Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kaijage amesema wamejiandaa vizuri kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni.

“Tumejiandaa, vijana wako vizuri wanasubiri saa ya mechi tu. Licha ya kwamba Afrika Kusini wako mbele kwenye mpira wa miguu wa wanawake si sababu ya matokeo,” amesema Kaijage.

Amesema anaamini vijana wake watafanya vizuri, na kuwataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kuwashangilia ili waweze kupata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na msisimko mkubwa.

Naye nahodha wa Tanzanite, Fatuma Issa amewataka Watanzania kuwaamini kwani wamejipanga kwa ajili ya pambano hilo, hivyo wawe nyuma yao katika kuwaongezea ari ili waweze kufanya vizuri.

Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000. Tiketi zitauzwa uwanjani katika magari maalumu.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.

No comments:

Post a Comment