Nyota wa zamani wa Barcelona Ronaldinho Gaucho ana matumaini ya kupata nafasi katika kikosi cha Brazil katika fainali ya kombe la dunia msimu wa majira ya kiangazi katika ardhi ya nyumbani nchini Brazil.
Kiungo huyo wa Atletico Mineiro ya Brazil mwenye umri wa miaka 33 kwa mara ya mwisho kuitumikia Selecao ilikuwa ni mwezi April alipojumuishwa kikosini katika mchezo dhidi ya Chile, lakini anaamini kuwa mauhusiano yake mazuri na kocha Luiz Felipe Scolari yanaweza kuwa chachu ya kuitwa kikosini endapo atakuwa katika kiwango bora.

"Ni mtu wa moja kwa moja na mara zote yuko muazi kwangu. Najua kuwa bado kuna nafasi kwa wale wenye kucheza vizuri " Alikuwa akiongea na mtandao rasmi wa fifa.com.
Mkataba wa Ronaldinho na Atletico Mineiro utamalizika mwishoni mwa mwezi huu wa Disemba.
No comments:
Post a Comment