Hatimaye Malawi imemwajiri Young Chimodzi kuwa kocha mkuu wa timu ya taufa na Jack Chamangwana kuwa msaidizi wake.
Inachukuliwa kama ni kujikosoa kwa chama cha soka cha nchi hiyo(FAM), ambacho mwezi Januari kiliwatimua kazini makocha hao kutoka katika benchi la ufundi la The Flames' technical panel'.
Rais wa FAM Walter Nyamilandu amesema wamefikiri kwa makini juu ya maamuzi hayo na kwamba wanaimani makocha hao watawafikisha fainali za Afrika mwaka 2015.
Chimodzi anajaza nafasi ya kocha wa zamani aliyeondoka raia wa Belgian Tom Saintfiet ambaye alifanya kazi ya kujitolea kabla ya kuondoka baada ya kushindwa kuifikisha Malawi katika fainali za kombe la dunia 2014.
Selikali ya Malawi imejidhatiti kuipatia FAM fungu Nyamilandu magumu yaliyo mbele yao yatadhoofishwa na hilo kuelekea kusaka nafasi ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika 2015.
No comments:
Post a Comment