Benchi la Ufundi la klabu ya Young Africans limesema limesikitishwa na taarifa
zilizoenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba wachezaji wao wawili kiungo Haruna Niyonzima na nahodha Nadir Haroub "Cannavaro"
walipigana katika mchezo dhidi ya Coastal Union siku ya jumatano jijini
Tanga na kudai kuwa habari hizo hazina ukweli wowote bali ni katika kutaka kuharibu twasira
ya timu.
Taarifa ya klabu hiyo iliyonukuliwa kupitia mtandao wa klabu hiyo ambazo zimemnukuu kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa zimesema kuwa benchi la ufundi limeshangazwa na taarifa hizo baada ya kuziona na
kuzisoma hii leo na kusisitiza walioandika wamefanya hivyo kwa ajili ya
maslahi yao tu.
Akinukuliwa Mkwasa amesema wameshangazwa na taarifa hizo kwani watu walikuwepo uwanjani na aliweza kushuhudia
mchezo huo, hakuna aliyeona Cannavaro na Niyonzima wakipigana katika
kipindi chote cha dakika 90 za mchezo, na kwamba washikwa na wasi wasi na waandishi
waliokuwepo uwanjani kama walikua makini kufuatilia mchezo na kuandika
kitu tofauti na walichokiona.
Akizidi kunukuliwa Mkwasa amesema Sheria za soka zipo wazi, mchezaji
au wachezaji wapigana ndani ya uwanja mwamuzi anawatoa nje ya uwanja kwa
kuwapa kadi nyekundu, sasa wameshangaa kuona taarifa hizo zilizoripotiwa
leo kuwa kuna wachezaji wao walipigana huku wachezaji wote
wakimaliza dakika 90 za mchezo huo.
Kuhusu
maandalizi ya mchezo wa jumapili Mkwasa amesema vijana wake leo
wamefanya mazoezi asubuhi kujiandaa na mchezo huo, na hakuna mchezaji
majeruhi hata mmoja kwani Hamis Kiiza, Hassana Dilunga waliokuwa
wagonjwa wameshaungana wenzao kambini na Athuman Idd "Chuji" aliyekua
amesimamishwa kurejeshwa kundini.
No comments:
Post a Comment