Difenda wa Ufaransa wa timu ya wachezaji wasiozidi miaka 21 Kurt
Zouma hii leo amekua gumzo kubwa katika harakati za kuwahi muda wa kufungwa kwa dirisha la usajili ambapo ndani ya masaa kadhaa hii leo amefanikiwa kujiunga na Chelsea akitokea St Etienne na punde tu akakabidhiwa akakabidhiwa tena kwa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama 'Ligue 1' kwa mkopo katika kipindi kilichosalia
cha msimu.
Taarifa hizi zimethibitishwa na klabu hiyo ya London.
Zouma mwenye umri wa miaka 19, alijiunga na akademi ya St Etienne akiwa na miaka 14, na
akawa mchezaji mtaalamu mwaka 2011 na anaonekana kama uwekezaji wa muda mrefu
wa Chelsea huku nahodha John Terry, 33, akikaribia mwisho wa uchezaji
wake katika klabu hiyo.
Chelsea wamethibitisha kupitia mtandao rasmi wa klabu hiyo wa (www.chelseafc.com) kwamba
walikuwa wamepata saini yake kwa mkataba wa miaka mitano na nusu.
Zouma ameichezea St Etienne michezo 52 katika ligi, michezo 12 msimu
huu, lakini alipigwa marufuku ya mechi 10 kwa kumchezea visivyo
mchezaji wa Sochaux Thomas Guerbert na kumvunja mguu pamoja na kutegua
kifundo chake cha mguu.
Mchezaji thabiti, Zouma alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa
kilichoshinda taji la dunia la U-20 kipindi kilichopita cha majira ya
joto na aliitwa na kocha Didier Deschamps kabla ya mechi ya kirafiki ya
Oktoba dhidi ya Australia ingawa hakucheza
.
Ripoti kwenye vyombo vya habari vilisema alinunuliwa takriban pauni
12.5 milioni ($20.62 milioni) na ndiye mchezaji wa tatu mkuu kujiunga na
Chelsea kipindi cha kuhama wachezaji cha Januari.
Nemanja Matic alijiunga nao kutoka Benfica na Mohamed Salah kutoka Basle huku Kevin de Bruyne na Juan Mata wakihama klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment