Afisa mtendaji wa Bodi ya ligi Silas Mwakibinga mwenye jezi nyekundu akiwa na mshambuliaji wa Mbeya City Mwigane Yeya. |
Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa sh. milioni 1.5 kwa kila klabu ya Ligi
Daraja la Kwanza (FDL).
Uamuzi
wa kuzisaidia timu hizo ulifanywa katika kikao cha TPLB kilichofanyika hivi
karibuni jijini Dar es Salaam ambapo fedha hizo zitalipwa kupitia kwenye
akaunti za klabu husika. Hivyo klabu ambazo hazijawasilisha akaunti zao TPLB
zinatakiwa kuwasilisha haraka.
Klabu
za FDL ni African Lyon, Burkina Moro, Friends Rangers, Green Warriors, Kanembwa
JKT, Kimondo, Kurugenzi Mafinga, Lipuli, Majimaji, Mkamba Rangers, Mlale JKT na
Mwadui.
Nyingine
ni Ndanda, Pamba, Polisi Dar es Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Morogoro,
Polisi Tabora, Stand United, Tessema, Toto Africans, Trans Camp na Villa Squad.
No comments:
Post a Comment