Nyota wa Zamani wa Simba, Yanga na Mtibwa Sugar Rashidi Gumbo |
Shirikisho
la Mpira wa Miguu la Shelisheli (SFF) limetuma Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) maombi ya Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa
wachezaji watatu wa Tanzania.
Wachezaji
walioombewa hati hiyo ili wakajiunge na timu ya La Passe FC inayocheza
Ligi Kuu nchini humo ni Salum Kinje aliyekuwa akiichezea timu ya Simba,
Semmy Kessy aliyekuwa Lipuli ya Iringa na Rashid Gumbo aliyekuwa timu ya
Mtibwa Sugar.
TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zitakapokamilika hati hizo zitatolewa.
No comments:
Post a Comment