Jumla ya wachezaji 20 wa timu ya taifa ya tanzani jioni ya
leo wameshiriki mazoezi ya timu hiyo ukiacha cholo ambaye ni majeruhi .
Mazoezi hayo yalioanza saa 11:30 yamemalizika saa 12:00
jiioni ambapo wachezaji walikuwa wakifurahia mazopezi hayo huku wakionyesha ari
kubwa ya kuinyoa Cameroon hapo kesho.
Akiongea mchana wa leo Poulsen amesema wachezaji wake wako
tayari kwa mchezo huo ambapo amesema katika mchezo huo amewaagiza wachezaji
kucheza kwa kasi, kujiamini na ikiwa ni pamoja na kutenganeza nafasi na
hatimaye kufunga magoli.
Amesema licha ya kwamba Cameroon inawachezaji wenye uzoefu,
nguvu na malengo bado Stars inanafasi ya kufanya vizuri endapo watacheza kwa
nafasi , mchezo wa kasi, kutengeneza nafasi na hatimaye kufunga magoli.
Poulsena amesema amefurahia sana kupata mchezo huo ambao
ameuita kuwa ni mchezo dhidi ya timu ngumu kama Cameroon baada ya jitihada za
pamoja baina ya TFF na wadhamini wa Stars Kilimanjaro na angependa kupata
michezo zaidi ya aina hiyo.
Kuhusu mchezo wa kesho amewataka wachezaji kucheza kwa
kujiamini na kuonyesha uwezo wao wote. Anaamini katika njia ambayo anapita
katika kuelekea kutafuta mwelekeo mzuri wa mafanikio ya timu na anaamini kwa
kushirikiana kwa pamoja mafanikio yako karibu kama mwenyewe anavyopenda
kuitumia kauli mbiu ya ‘Umoja ni nguvu’
kwani mchezo wa mpira wa miguu ni rahisi na wachezaji wake wako tayari kwa
hilo.
Bofya kumsikiliza.
Bofya kumsikiliza.
No comments:
Post a Comment