Kinda wa Manchester United Adnan Januzaj huenda kaanza kuichezea timu yake ya taifa kwa mara ya kwanza baada ya kualikwa kuichezea Kosovo mwezi March.
Januzaj mzaliwa Belgium mwenye wazazi raia mchanganyiko wa Kosova na Albanian amekuwa ni mmoja wa wachezaji wazuri dunaini mara baada ya kuanza kuicheza soka Old Trafford.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 anaonekana kutakiwa na mataifa kadhaa wakiwemo England, Serbia, Albania, Turkey, Croatia na Belgium.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 anaonekana kutakiwa na mataifa kadhaa wakiwemo England, Serbia, Albania, Turkey, Croatia na Belgium.
Meneja wa England Roy Hodgson amekuwa akihaha kupata huduma ya Januzaj, ambaye anaweza kufuzu kuichezea timu atakapo fikisha umri wa miaka 23.
Chini ya sheria ya Fifa inasema kuwa mchezaji anaweza kulichezea taifa lolote endapo atakuwa amekamilisha kucheza soka ndani ya taifa hilo kwa kipindi cha miaka mitano kabla ya kuliwakilisha.
Lakini Kosovo wanamatumaini ya kupata huduma ya winga huyo kwa mara ta kwanza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Haiti .
No comments:
Post a Comment