Hatma ya baadaye ya Robin van Persie ndani ya Manchester United inaendelea kuonekana kuwa katika hali ya wasiwasi ilhali wiki za hivi karibuni kuna dalili za mshambliaji huyo kuchukua nafasi ya Nemanja Vidic katika nafasi ya unahodha.
Mshambuliaji huyo mduchi ambaye kwasasa ni skipper katika kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi amekuwa katika orodha ya watu wa mbele kuchukua nafasi ya kitambaa cha unahodha kuanzia msimu ujao baada ya kuthibitika kuwa Vidic ataondoka katika klabu hiyo wakati wa kiangazi.
Hata hivyo tayari mtandao wa United umeorodhesha majina matano ambayo yanaweza kuchukua unahodha ambapo jina la Van Persie halipo.
Katika orodha hiyo lipo jina la Wayne Rooney ambaye anatarajiwa kuongeza muda wa kuichezea klabu hiyo sambamba na majina ya David De Gea, Jonny Evans, Phil Jones na Darren Fletcher.
Van
Persie bado anayo nafasi bado ya kupata nafasi hiyo kwani inakumbukwa mwaka uliopita aliwahi kuwa nahodha katika kikosi cha Arsenal, ilhali pia inakumbukwa alikua nahodha katika safari ya United katika ziara ta mashariki ya mbali wakati wa kiangazi.
Bado kumekuwepo na taarifa kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 hajatulia ndani ya Old
Trafford iliyochini ya meneja David Moyes. Alikuwa benchi katika kipindi cha wiki sita kutoka na kuwa majeruhi katika kipindi cha mwezi Disemba kuelekea mwaka mpya na anaendelea kupigania kiwango kurejesha kiwango cha msimu uliopita.
Patrice
Evra, pia hayupo katika orodha hiyo na anaweza akaondoka ndani ya klabu hiyo kama ilivyo kwa Vidic baada ya kumalizika msimu.
Orodha fupi ya majina kupitia mtandao wa United kama inavyoonekana
Vidic kushoto juu amethibisha kuondoka United kiangazi huku hatma ya Van Persie pichani juu kulia ikiwa bado tete.
No comments:
Post a Comment