KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, February 2, 2014

Banana Zoro, JB, Irene Uwoya, Mboto, Blandina Chagula wakabidhiwa kadi za chama tawala na kuserebuaka mbaya uwanja wa Sokoine Mbeya.Hawa hapa..

Matumizi ya wasanii katika tambo za kisiasa nchini yameendelea kuchanua leo baada ya wasanii kadhaa wa Bongo Movie, kukabidhiwa kadi za CCM, jijini Mbeya.
Hatua hii imekuja ikiwa ni miezi michache tu baada ya wapinzani wakuu nchini CHADEMA, kutangaza lundo la wasanii ambao wamejiunga na chama chao akiwemo Suleyman Msindi (Afande Sele) na Joseph Haule (Profesa J)
Katika kujibu mapigo ya wapinzani wao, Chama cha Mapinduzi, leo kikatumia maadhimisho ya miaka yake 37 toka kuzaliwa kwa chama hicho, kuwakabidhi kadi za uanachama wasanii kadhaa wenye majina makubwa nchini, akiwemo mwimbaji mahiri Banana Zoro.
Mbali yake, wasanii Irene Uwoya, Blandina Chagula, Jacob Steven (JB), Mboto na wengine, walikabidhiwa kadi na mwenyekiti wa CCM Taifa, ambaye pia ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Mbeya kitaifa.

No comments:

Post a Comment