KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, February 10, 2014

Coastal yawatoa hofu mashabiki kuelekea katika michezo ijayo ya ligi

Baada ya ushindi wa jana katika mechi ya jana Rhino Rangers na Coastal Union kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, ambapo Jerry Santo aliipatia Coastal Union bao la mapema dakika ya pili, Coastal Union imepanda mpaka nafasi ya tano.
Kwa mujibu wa msimamo wa ligi, Coastal Union kabla ya ushindi wa jana ilikuwa na point 19 katika nafasi ya saba. Baada ya Mtibwa Sugar kupoteza mchezo wake dhidi ya Mbeya City, wameendelea kubaki na point 22, ambazo Coastal pia wamezifikia hivyo kuwafanya kushuka nafasi moja chini kutokana na tofauti ya mabao ya kushinda na kushindwa.
Hivyo habari njema kwa mashabiki wa Coastal Union, ni kuwa kwa sasa Coastal wanasema wanaendelea na wimbi la ushindi ili kujeweka katika nafasi nzuri hasa ikizingatiwa kocha ameamua kufanya mabadiliko ya kikosi chake ili kupata ushindi kila mechi inayokuja.
Anaeshika nafasi ya kwanza ana point 36, na sisi kutokana na mechi tisa tulizobakisha ikiwa tutashinda zote tutakuwa na jumla ya point 49. Kwa maana hiyo uwezekano wa kumaliza nafasi tatu za juu upo ikiwa tutafanya vizuri katika mechi tisa tulizobakisha ambazo ni dhidi ya:
Simba, Kagera Sugar, Azam FC, Mgambo JKT, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Ashanti, Mtibwa Sugar na Mbeya City.  
Ikumbukwe kuwa mechi tatu za awali kabla ya leo kukutana na Rhino Rangers tulivaana na JKT Oljoro (1-1), Yanga (0-0) na Tanzania Prisons (0-0).

No comments:

Post a Comment