Kocha wa Nigeria Stephen Keshi, amewajumuisha
wachezaji watatu ambao hawajawahi kuichezea timu ya taifa ya nchi hiyo
Super Eagles, katika kikosi chake kitakachochuana na Mexico, mjini
Georgia, Atlanta tarehe tano mwezi ujao, katika mechi ya kimataifa ya
kirafiki.
Wachezaji hao ni pamoja na Imoh Ezekiel, Ramon Azeez na Michael Uchebo
Mshambulizi
matata wa Standard Liege Imoh Ezekiel, sasa amepewa fursa ya
kujitafutia nafasi katika kikosi cha Nigeria, kitakacho wakilisha taifa
hilo kwenye fainali ya kombe la dunia nchini Brazil.
Msimu huu Ezekiel, mwenye umri wa miaka 20,
amefunga magoli tisa na kwa muda mmrefu amekuwa katika hali nzuri hali
iliyomfanya kocha Keshi kumjumuisha kwenye kikosi chake.
Uchebo, ambaye anasakata soka nchini Ubelgiji,
ameifunguia klabu klabu yake ya Cercle Brugge amegoli matano naye mcheza
kiungo Azeez kwa upande wake hajakuwa na bahati ila amekuwa miongoni
mwa wachezaji ambao wanauwezo wa kucheza safu ya kati na ushambulizi kwa
wakati mmoja.
Wachezaji wawili wa kutegemewa wa Nigeria, Shola
Ameobi wa NewCastle na Brown Ideye wa Dynamo Kiev kwa sasa wako chini
kimchezo na aliyekuwa mshambulizi wa timu ya taifa ya Nigeria Uchebo
huenda akajikatia tikiti ya kwenda Brazil.
No comments:
Post a Comment