Viongozi wa Kamati ya Olimpiki duniani wameirejeshea
India kiti chake katika kamati ya olimpiki duniani (IOC)baada ya
kutimuliwa yapata mwaka mmoja uliopita.
India ilipigwa marufuku kutokana na shtuma kuwa ilikuwa imeingilia kati uchaguzi wa kitaifa wa kamati ya olimpiki nchini humo .
Kamati ya Olimpiki duniani iliagiza kufanyike
mabadiliko ya katiba ya shirikisho la India mbali na kuruhusu uchaguzi
huru na wa haki kufanyika.
Hata hivyo kurejeshwa kwa India haitakuwa afueni
kwa wanariadha kutoka taifa hilo wanaoshiriki mashindano ya olimpiki ya
msimu wa baridi huko Sochi Urusi chini ya bendera ya Kamati ya Olimpiki
duniani wala sio ile ya India .
No comments:
Post a Comment