Botswana inatarajiwa kumteua Peter Butler kutoka Uingereza kuwa kocha wake mpya wa timu ya taifa ya soka.
Shirikisho la mchezo wa soka nchini Botswana,
limesema kuwa litakuwa na habari muhimu siku ya Jumatano wakati wa kikao
chake na waandishi wa habari mjini Gaborone
Inatarajiwa
kuwa Butler mwenye umri wa miaka 47, atatangazwa kuwa kocha mpya naye
Benny Kgomela akiteuliwa kuwa mkurugenzi wa masuala ya kiufundi.
Ripoti zinasema kuwa Butler, amesaini mkataba wa
miaka miwili na shirikisho hilo, kuchukua mahala na Stanley Tshosane
ambaye alifutwa kazi Oktoba mwaka uliopita.
Tshosane ndiye kocha wa kwanza kuwahi kuongoza
timu ya taifa ya soka ya Botswana kufuzu kwa fainali za kuwania kombe la
Mataifa Bingwa barani Afrika mwaka wa 2012, lakini alifutwa kazi baada
ya timu hiyo kuandikisha matokeo mabaya mwaka uliopita.
Baada ya ya miezi minne ya uteuzi wa kocha mpya,
shirikisho la soka nchini Botswana lilimchagua Butler, licha ya wengi
kumpigia upato kocha mkuu wa timu ya taifa ta Uganda, Milutin
Sredojevic.
No comments:
Post a Comment