Mechi ya ligi kuu ya Premier kati ya Fulham na
Liverpool siku ya Jumatano, huenda ikahairishwa ikiwa mgomo wa
wafanyakazi wa treni mjini London utaendelea kama ulivyopangwa.
Wafanyakazi hao wa treni wanatarajiwa kuanza
mgomo wa saa 48 kuanzia leo, hali ambayo inaweza kutatiza shughuli za
usafiri kama ilivyokuwa wiki iliyopita mjini humo.
Wasimamizi
wa Fulham wana wasi wasi kuwa wafanyakazi wao huenda washindwe kufika
kazini kwa muda unaofaa au hata kukosa kufika ili kuhakikisha kuwa mechi
hiyo inaendelea.
Klabu hiyo inatarajiwa kutangaza baadaye hii leo ikiwa mechi hiyo itahairishwa au la.
Wamiliki wa klabu hiyo wamekuwa na mazungumzo na
maafisa wa baraza la mji wa London pamoja na maafisa wa polisi na
wamesema kuwa wana matumaini kuwa mechi hiyo itachezwa kama
ilivyopangwa.
Huku hayo yakijiri, leo hii kutakuwa na mechi kadhaa za ligi kuu ya premier.
Cardif City itakuwa mwenyeji wa Aston Villa, Southampton kusafiri ugenini kucheza na Hull City.
West Ham itakuwa nyumbani kutoana jasho na
Norwich, ili hali West Brom kualika vinara wa ligi hiyo kwa sasa Chelsea
katika uwanja wao wa nyumbani.
No comments:
Post a Comment