Klabu ya Lazio imetoa taarifa rasmi za kiofisi yaani (official documents) kuthibitisha kuwa kiungo mwenye umri wa miaka 17Joseph Minala si kweli kuwa ana umria wa miaka 41.
Minala aliibua mjadala mkubwa wiki hii kutokana na muonekana wake baada ya kutokea taarifa hizo za kizushi kuwa Lazio imekuwa katika mpango wa kumpromoti katika kikosi cha kwanza akiwa ni -youngest players- katika miaka ya hivi karibuni kuwemo katika kikosi cha kwanza cha Lazio.
Amekuwa akikumbana na maneno mengi ya kashfa ambayo yamekuwa yakipitia mitandao ya kijamii huku shutuma nyingi zikidai kuwa amekuwa mdanganyifu wa umri ambapo imekuwa ikiarifiwa kuwa ana umri mkubwa sana zaidi ya umri wake halisi wa miaka 17.
Wakala wa Minala amepingana na taarifa hizo lakini taarifa zikiibuka zaidi katika vyombo vya habari vya nchini Senegal kwa madai kuwa mchezaji huyo kwasasa ana umri wa miaka 41 na itakapo fika mwezi Ogasti atakuwa anafikia umri wa miaka 42.
Madai ni kuwa amekuwa akidanganya umri ili aweze kulipwa pesa nyingi na kutuma kwao katika familia yake nchini Cameroon.
Hata hivyo, Lazio imeweza kumaliza tetesi hizo kwa kuchapisha taarifa zake rasmi katika mtandao wa klabu hiyo huku klabu hiyo ikisisitiza kuwa 'registration' imedhihirisha kuwa kiungo huyo ni kweli ana umri wa miaka 17.
No comments:
Post a Comment