Serikali ya Marekani imeonya mashirika ya ndege
yanayofanya safari za kwenda Urussi kwamba magaidi huenda wakajaribu
kuingiza kimagendo vilipuzi vilivyofichwa ndani ya neli za dawa ya
kusugua meno.
Afisa mmoja wa idara ya usalama nchini Marekani
amesema vifaa kama hivyo huenda vikatumiwa kujenga bomu ndani ya ndege
au baada ya kuwasili katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi
ambayo yataanza Ijumaa katika mji wa milimani wa Sochi.
Afisa huyo hata hivyo alisema kuwa
serikali yake haina ushahidi wa tishio la moja kwa moja wa mashindano
hayo ya Olimpiki ya Sochi .
Vikosi vya usalama vya Serikali ya Urussi viko
katika hali ya tahadhari kuu baada ya makundi ya wanamgambo na magaidi
kutishia kufanya mashambulizi katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa
baridi ya Sochi.
Dagestan
Vikosi vya usalama katika jimbo la Dagestan
nchini Urussi vimemuua kwa kumpiga risasi mwanamgambo wa kiislamu katika
mji wa Izberbash.
Dzhamaldin Mirzayev mwenye umri wa miaka
thelathini anashukiwa kuandaa mashambulizi ya bomu ya kujitoa mhanga
katika mji wa Volgograd mwezi Disemba.
Watu thelathini na wanne waliwauwa katika shambulizi hilo.
Inadhaniwa kuwa Mirzayev ndiye aliyewapa mafunzo washambulizi wawili wa kujitoa mhanga .
No comments:
Post a Comment