Edinson Cavani amekuwa akivutia vilabu vya Premier League kama Chelsea na Manchester United |
Wawakilishi wa Edinson Cavani wako jijini London hii leo wakati huu ambapo mshambuliaji huyo akiwa katika fikira za kuihama klabu yake ya Paris Saint-Germain wakati wa kiangazi.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay kwasasa ana anatibu majeraha ya paja ambayo inaarifiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja katika mchezo ujao wa vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen.
Amekuwa katika mafanikio katika timu yake ambayo ni mambingwa waa taji la Ufaransa lakini pia anaonekana kutokuwa na hakika katika maisha yake ya baadaye na anaonekana si mwenye furaha ukimtazama kupia macho kwa nje (yaani 'body language') wakati huu ambapo amekuwa akishirikiana vema na Zlatan Ibrahimovic katika safu ya ushambuliaji.
Cavani amekuwa katika mafanikio tangu ajiunge na PSG akitokea Serie A katika klabu ya Napoli kwa ada ya pauni milioni £54.
Taarifa zinaarifu kuwa Manchester United ilikuwa ikimsaka Cavani wakati huo ambapo Sir Alex Ferguson
alikuwa akifanya mazungumzo na Laurent Blanc kusaka uwezekano wa kupatikana kwa mwezi uliopita.
United inasalia kuwa katika harakati za kumpata mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 lakini kwasasa inaonekana pia Chelsea nao wameingia katika kinyang'anyiro hicho.
Vilabu vyote hivyo vinaoenaka kuwa na orodha ya wachezaji zinazofanana huku bosi wa Blues Jose Mourinho
akiwa mbelea kutaka huduma ya Diego Costa wa Atletico Madrid pamoja na Mario Mandzukic wa Bayern Munich.
No comments:
Post a Comment