Laudrup aliye na hasira kali baada ya kutimuliwa kazi ametishia kuelekea kwenye mkondo wa sheria akidai kuwa klabu yake iliyomtimua kazi ya Swansea haikumpa sababu ya kwanini wamemtimua kazi na Dane hakumruhusu hata kwenda kuwapa mkiono wa kwaheri wachezaji wa klabu hiyo.
- Michael Laudrup alifutwa kazi na Swansea Jumanne usiku.
- Laudrup hakupewa nafasi ya kuwaaga wachezaji na stafu wengine.
- Dane alipewa taarifa ya kutimuliwa kazi kupitia chama cha mameneja wa ligi (League Managers Association)
- Garry Monk kwasasa ndiye meneja wa muda wakati huu ikiwa katika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi.
The Dane alishinda Capital One Cup akiwa na Swans msimu uliopita.
Na Laudrup amepitia njia hiyohiyo kuwasilisha taarifa ya masikitiko yake ya namna alivyofanyiwa.
Taarifa iliyopitia kwa chama cha mameneja wa ligi ilisomeka kama ifuatavyo
‘kwa kweli nimehuzunishwa na kuondolewa kazini kama meneja wa Swansea City.
'kwakweli kwa namna ambayo ilivyofanyika na maamuzi ya yaliyofanywa na klabu tangu nilipopewa notice hiyo katika taarifa fupi ya maandishi ambayo haikunipa sababu kwani nimefukuzwa kazi nimeshindwa kuelewa kwanini imefanyika hivyo.
'nimepata ushauri wa kisheria na tayari kwa kushirikiana na LMA tayari wameiandikia klabu hiyo juu ya kutaka maelezo zaidi.
No comments:
Post a Comment