Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini amethibtisha kuwa mshambuliaji wake Sergio Aguero hatacheza katika mchezo wa kesho wa kwanza wa ligi ya mabingwa Ulaya wa hatua ya 16 bora dhidi ya Barcelona.
Msimu huu kwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina umekuwa aukikumbwa na majeraha ya hapa na pale huku jeraha lingine la hivi karibuni akilipata katika wa ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya Tottenham mwezi uliopita akiumia muda mfupi baada ya kufunga goli la kwanza.
Pellegrini alikuwa ni mwenye matumaini ya kuwa na mshambuliaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid katika benchi lake la wachezaji wa akiba wakati watakapokuwa ugenini dhidi ya kikosi cha Tata Martino baada ya kuimarisha afya yake na wiki iliyopita akifanya mazoezi katika kikosi cha kwanza.
Hata hivyo taarifa za hii leo kupitia kwa meneja wa Barcelona Martino Tata mwenye zimearifu kuwa na hapa nanukuu
"Aguero hayupo katika kikosi. Tunajaribu kuangalia kama atakuwa fiti kwenye wa Jumamosi dhidi ya Stoke lakini pia huenda ikawa ni ngumu."
Aguero amefunga jumla ya magoli 26 katika jumla ya michezo 25 ya msimu huu yakiwemo magoli sita ya ligi ya mabingwa
Aguero amefunga jumla ya magoli 26 katika jumla ya michezo 25 ya msimu huu yakiwemo magoli sita ya ligi ya mabingwa
Pia Pellegrini, ana matumaini ya kumtumia kiungo Fernandinho baada ya kurejea kutoka katika maumivu ni baada ya kukosekana kwa takribani michezo mitatu.
No comments:
Post a Comment