Mlinzi wa kushoto wa Swansea Ben Davies (pichani kushoto) yuko katika mawindo ya vilabu vingi Ulaya |
Mlinzi wa Swansea Ben Davies ameelezea kutakiwa na vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya licha ya kusaini mkataba mkataba wa miaka minne na nusu kabla ya Christmas.
Mlinzi huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri miaka 20 alikuwa akiwindwa na Manchester City,
Liverpool, Arsenal na kwa mshangao mkubwa pia Atletico Madrid ilikuwa ikimuwinda katika siku za hivi karibuni.
Vilabu vyote hivyo vimeingia sokoni hivi sasa kusaka mlinzi wa kushoto
Davies amecheza zaidi ya michezo 60 tangu ajiunge na Swansea na akicheza mchezo wa kwanza katika mchezo dhidi ya West Ham mwezi Agosti 2012 ambapo uwezo wake umekuwa ukiongezeka kwa kasi.
Swansea
imekuwa haitaki kumuuza mlinzi huyo na imekuwa ikionyesha uwezo wa kupingana na ofa kadhaa ikiwemo ya Fulham
ambayo ilikuwa mpango mezani wa pauni milioni £4 wakimtaka mchezaji mwenzake na Davies huyu si mwingine bali ni Neil Taylor mwezi uliopita.
Davies (kulia) amekuwa akivutia licha ya uwezo mdogo wa klabu yake katika Premier League msimu huu
No comments:
Post a Comment