Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekubali kukiweka kikosi chake katika hatari zaidi kimatokeo kwa kuwapumzisha baadhi ya wachezaji muhimu katika mchezo wa keshokutwa wa michuano ya FA dhidi ya Liverpool kwa matumaini ya kuichapa Bayern Munich ambao ni mabingwa wa Ulaya.
Mshabiki wa Gunners wanaamini kuwa FA Cup ndio michuano ambayo inastahili kuwekewa kipau mbele msimu huu kwani ndhiyo taji pekee lililo wazi kwa upande wao waqkati huu ambapo inaonekana ligi kuu ya Englang 'Premier League' na vilabu bingwa Ulaya kuonekana kama ni michuano migumu kwa wakati huu na mchezo dhidi ya Munich pia kuonekana kuwa ni mgumu kwa upande wao.
Lakini Wenger hakubali na hilo ambapo amedhamiria kuwapumzisha nyota wake kadhaa muhimu katika mchezo wa kesho kutwa dhidi ya Liverpool Jumapili licha ya kumbukumbu ya kichapo cha mabao 5-1 kikiwa bado hakijasahauliwa na mashabikiwa wa klabu hiyo.
Taarifa zinaarifu kuwa meneja huyo mfaransa huenda akawapumzisha mlinda mlango wake namba moja Wojciech Szczesny, Olivier Giroud, Mesut Ozil na Mikel Arteta, huku makinda kama Serge Gnabry na Carl Jenkinson pamoja na Nicklas Bendtner na Lukasz Fabianski wakitarajiwa kuanza kikosini dhidi ya Liverpool.
No comments:
Post a Comment