Young Africans kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wa marudiano
dhidi ya timu ya Komorozine de Domoni ya Anjuan Visiwa vya Comoro katika
mchezo wa Klabu Bingwa Barani Afrika utakaofanyika mji wa Mitsamihuli
kwenye uwanja wa Sheikh Said Mohamed International kuanzia majira ya 9
kamili mchana kwa saa za Afrika Mashariki.
Mara baada ya jana jioni kufanya mazoezi mepesi katika uwanja mdogo
wa hotel ya Retaj, leo kikosi cha Young Africans kimeweza kufanya
mazoezi asubuhi majira ya saa 5 ausbuhi katika Uwanja wa Sheikh Said kwa
ajili ya kuuzoea tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho.
Kocha mkuu
wa Young Africans Hans Van der Pluijm amesema anashukuru kikosi chake
kipo vizuri kuelekea mchezo huo na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja
hivyo anapata fursa ya kuchagua amtumie nani katika mchezo huo.
Akiongelea
wapinzani timu ya Komorozine de Domoni amesema hawajaidharaua mechi ya
kesho kama watu wengi wanavyofikiria, kikubwa amewaandaa vijana wake
waeze kufanya vizuri na kupata ushindi, "Kwangu mie hakuna mechi ndogo
wala mchezo wa kirafiki" alisema Hans.
Young Africans itashuka
dimbani kucheza mchezo huo wa marudiano ikiwa na kumbukumbu nzuri ya
ushindi wa mabao 7-0 iliyoupata katika mchezo wa awali uliofanyika
jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment