Mkimbiaji katika barafu wa Ujerumani katika michezo ya Sochi |
Na katika michezo ya olimpiki ya Sochi, kamati ya kimataifa ya Olimpiki imewakaripia wanariadha kwa kuvaa jezi zenye ujumbe wa kukumbuku ya watu waliofariki. Msemaji wa IOC Mark Adams amesema leo kuwa kamati ya olimpiki imetuma barua katika kamati ya olimpiki ya Norway baada ya mwanariadha wake wa mbio za kuteleza katika barafu kuvaa kitambaa cheusi siku ya Jumamosi akimkumbuka mchezaji mwenzake ambaye ni kaka yake, aliyefariki katika mkesha wa michezo ya Sochi.
Wakati huo huo Norway inaongoza msimamo wa medali katika michezo hiyo ya
olimpiki ya Sochi ya majira ya baridi kwa kuwa na jumla ya medali 7 ,
mbili za dhahabu, moja ya fedhja na nne za shaba. Inafuatiwa na Uholanzi
yenye jumla ya medali 4 , mbili ziikiwa za dhahabu. Ujerumani iko
nafasi ya 5 ikiwa na medali mbili za dhahabu.
No comments:
Post a Comment